Mfahamu Brian Deacon, Muigizaji wa filamu ya Yesu aliyeishi maisha ya kipagani na baadae kuokoka
Muigizaji wa filamu, Brian Deacon ambaye ndiye aliyeigiza filamu ya Yesu (Jesus) alizaliwa mnamo tarehe 13/02/1949 huko Oxford nchini Uingereza akiwa ni mtoto wa pili katika familia yao, baba yake akiwa fundi makenika na mama yake akiwa ni Nesi. Brian alipita kwenye mchujo mkali wa waigizaji zaidi ya 1000 ambao walifanyiwa mahojiano huku 260 wakijaribishwa kuigiza (screen test) kuona kwamba wanafaa, ambapo yeye akiwa ni mwingereza pekee kati ya waigizaji Waisrael walioingia kwenye usaili huo akiwa chini ya kampuni iitwayo New shakespears ambako alikuwa akifanya sanaa za majukwaani na uigizaji. Akihojiwa na BBC, Brian amesema kabla ya kuchaguliwa mtihani wake wa kwanza ulikuwa kutoka kwa wakala wake aliyemvunja moyo kwa kumweleza kuwa kama ataweza kuigiza kama Yesu. Hata hivyo, baadae alifanikiwa na baada ya hapo akawa na wakati mgumu kutoka kwa watu ambao kila mmoja alikuwa anajaribu kumweleza jinsi anavyotakiwa kuigiza sauti yake na mambo mengine, ingawa yeye alisema atatumia sau...